UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

26 Oct, 2025 12 Machapisho
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 
Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.

Akiwa katika mkutano wa uhamasishaji wa wananchi kujitokeza kupiga kura, Ndg. Martine alieleza kuwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, kupitia ongezeko kubwa la mikopo isiyo na riba kutoka Halmashauri kwa makundi maalum ya kijamii:

Wanawake: TZS Bilioni 99
Vijana: TZS Bilioni 96
Walemavu: TZS Bilioni 45.

 “Mikopo hii ni ushahidi tosha kwamba Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza kwa vitendo dhamira ya kuwawezesha Watanzania kiuchumi. Hivyo tarehe 29 Oktoba, ni lazima kila kijana na kila mfanyabiashara atoke na kitambulisho chake cha mpiga kura kwenda kutiki NDIYO kwa CCM,” alisema Martine.

Aliwasisitiza wananchi wote kubeba vitambulisho vya wapiga kura, kujitokeza mapema vituoni  na kuhakikisha wanampigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais, pamoja na wagombea wa Ubunge na Udiwani kutoka CCM, ili kuendeleza kasi ya maendeleo na ustawi wa Taifa.

#TokaNitokeTukatiki ✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele 
#TunazimaZoteTunawashaKijani 
#FyuchaBilaStresi