UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

WANAVYUO LINDENI AMANI NA UTULIVU MTAKAPOFUNGUA VYUO, KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KULINDA AMANI NA UTULIVU NCHINI TANZANIA

12 Nov, 2025 30 Machapisho
Ndg. Emanuel Martine
Upanga, Dar es Salaam

Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa, Ndg. Emanuel Martine, leo tarehe 12.11.2025 amefanya mazungumzo na wanavyuo mbalimbali waliofika kumtembelea katika ofisi za Upanga, jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Ndg. Martine amewaomba wanavyuo hao na wanavyuo wote nchini kuhakikisha kila mmoja katika chuo chake analinda amani na utulivu vyuoni na nchini kwa ujumla, watakapofungua vyuo, na kusoma kwa bidii kwa manufaa ya Tanzania.

Martine amesema, “Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutekeleza utoaji wa mikopo kwa wanavyuo wa vyuo vya kati na vyuo vikuu. Kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na taasisi zote zilizopo chini yake, Serikali imejipanga vyema kuwahudumia wanavyuo katika vyuo vyao, zikiwemo menejimenti za vyuo.”

Ameongeza kuwa, “Serikali imetenga Bilioni 916.5 kugharamia masomo ya wanavyuo wa vyuo vya kati, vyuo vikuu, na wale wa ufadhili wa Samia Scholarship pamoja na Samia Extended Program. Aidha, Serikali inaendelea kutoa elimu bila ada kwa kidato cha tano na cha sita. Hivyo, wanavyuo wote wanapaswa kuwa watulivu nyakati zote kwani Serikali imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, ikiwemo ongezeko maradufu la bajeti ya mikopo kutoka Bilioni 464 mwaka 2020/2021 hadi Bilioni 916.5 mwaka 2025/2026.”

“Ndoto, maono na mawazo tuliyonayo kama vijana yatatimia na kufanikiwa endapo kuna ustawi wa amani katika nchi yetu. Amani hii tuitunze kama mboni ya jicho kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu.”

“Amani ya Tanzania tunapaswa kuilinda sote kwa pamoja. Amani ni msingi wa maendeleo ya taifa letu. Wanavyuo, lindeni amani na utulivu vyuoni mtakapofungua vyuo.”

#WanavyuoLindeniAmaniNaUtulivuVyuoni
#KaziNaUtuTunasongaMbele