UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

HOTUBA FUPI YA WAZIRI MKUU MTEULE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

13 Nov, 2025 30 Machapisho
Waziri Mkuu mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba baada ya kupitishwa kwa kishindo na wabunge alipata wasaa wa kuhutubia kwa uchache.

Katika hotuba yake fupi Dkt. Mwigulu alitumia muda huo kumpongeza dkt. Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa ujumla. Kupitia pongezi hizi alikumbusha kuwa,

"Katika miaka mitano, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejitambulisha kuwa ni Rais anayetaka matokeo ya haraka yanayotatua matatizo ya watazania" 

Dkt. Mwigulu anatarajiwa kuapishwa rasmi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho tarehe 14 Novemba, 2025 Ikulu Chamwino, Dodoma kuanzia Saa 4:00 Asubuhi.

#KaziNaUtuTunasongaMbele