UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

HOTUBA YA KIHISTORIA YA DKT SAMIA KUFUNGUA BUNGE LA 13 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

13 Nov, 2025 21 Machapisho
Ni tukio lenye uzito wa kipekee katika historia ya Taifa letu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua rasmi Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho, tarehe 14 Novemba 2025, kuanzia saa 9 alasiri, bungeni Dodoma.

Hotuba hii inasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wote, ikitarajiwa kuelekeza dira ya Maendeleo, umoja na mageuzi katika sekta zote muhimu za Taifa. 

Ni wakati wa kutazama mbele kwa matumaini mapya, kasi mpya na mwelekeo mpya wa ujenzi wa Tanzania yenye uchumi Imara, watu wenye ustawi, na uongozi wa uwazi na uadilifu.

Kupitia tukio hili, Taifa linafungua ukurasa mpya wa safari ya pamoja safari ya kuimarisha demokrasia, kujenga uchumi shindani na kulinda amani tuliyonayo.