UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SERIKALI CHINI YA RAIS DKT.SAMIA KUANZISHA WIZARA KAMILI YA VIJANA

14 Nov, 2025 51 Machapisho
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita imedhamiria kuanzisha Wizara kamili itakayoshughulikia masuala yote yanayohusiana na Vijana.

Akizungumza wakati akihutubia katika ufunguzi wa Bunge la 13 la Tanzania leo tarehe 14 Novemba 2025 Jijini Dodoma, Rais Dkt. Samia amesema anatarajia kuwa na Washauri wa Rais watakaomshauri kuhusu mambo ya Vijana ikiwemo changamoto zao.

Mimi na wenzangu katika Serikali tumefikiria kuwa na Wizara kamili itakayoshughulikia mambo ya Vijana

Tumeamua kuwa na Wizara kamili badala ya kuwa na Idara iliyo na mambo mengi

Vilevile nafikiria kuwa na Washauri wa mausala ya Vijana ndani ya Ofisi ya Rais