UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Tanzania kunufaika na dolla million 20 kwa utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mbadiliko ya Tabia ya nchi

15 Nov, 2025 42 Machapisho
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotarajia kunufaika na fedha kiasi cha hadi dola milioni 20 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Mfuko wa Kukabiliana na Hasara na Uharibifu.
 
Hayo yamesemwa na Mshauri wa Rais katika masuala ya Mazingira na Mwenyekiti wa Kundi la Majadiliano la Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (AGN) Dkt. Richard Muyungi alipokutana na Watanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa wa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.
 
Dkt. Muyungi amesema kuwa katika utekelezaji huo tayari zimetengwa fedha kiasi cha dola milioni 250 kwa mwaka ujao kwa kwa ajili ya kufadhili miradi hiyo ambayo Tanzania ni nchi mnufaika.
 
“Nasisitiza huu sio mkopo bali ni ufadhili na hadi sasa tuna mambo ya kufuatilia na sisi kama nchi tumepewa kipaumebele hivyo tunaweza kuwa na miradi hata miwili ambayo inaweza kuwa na manufaa makubwa, naomba Ofisi ya Makamu wa Rais tuteua mtu mmoja yaani focal person kwa ajili ya Mfuko wa Kukabiliana na Hasara na Uharibifu,” amesema.
 
Kubwa zaidi amebainisha kuwa mwaka 2025 Tanzania imeteuliwa kuwa Kituo cha Santiago ambacho kitakuwa kinaratibu msaada wa kiufundi kwa nchi zinazoathiriwa na hasara na uharibifu unaotokana na mabadiliko ya tabianchi. 
 
Aidha, Dkt. Muyungi ameomba Watanzania kutoka serikalini na sekta binafsi wanaoshiriki mkutano huo wenye takriban washriki 60,000 kusimama kama nchi na kujenga mitandao ya kuchangamkia fursa ili kuendelea kuinufaisha nchi.  
 
“Kama tunavyoona hapa COP 30 yapo mabanda mengi yenye wingi wa washiriki nawaomba tutumie fursa hii kutengeneza network, tuna timu ya negotiation tufuatilie fursa za benki , NGOs na Serikali ili tukitoka hapa tutoke na faida,” amesisitiza. 
 
Vilevile, Dkt. Muyungi alitumia nafasi hiyo kuwaeleza washiriki hao kuwa wana jukumu la kuitangaza Dira ya Maendeleo 2025 na Serikali ya Tanzania imetekeleza mambo gani ya msingi kwa wananchi na hivyo kuchagiza upatikanaji wa fursa zaidi kwa maendeleo