UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

RAIS SAMIA AWATAKIA HERI WANAFUNZI WANAOHITIMU KIDATO CHA NNE

17 Nov, 2025 54 Machapisho

Rais Dkt. Samia amewatakia heri na baraka wanafunzi 595,816 wa Kidato cha Nne wanaoanza mtihani wa kuhitimu leo tarehe 17 Nov, 2025  katika shule 5,868 nchini.

Amesisitiza kuwa, pamoja na juhudi za Serikali za kujenga miundombinu, shule 305 mpya zinafanya mtihani huu kwa mara ya kwanza mwaka huu 2025  hatua inayothibitisha dhamira ya Serikali ya kupanua fursa za elimu bora kwa watoto wote wa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameandika:-
*"Ninawatakia kila la kheri wanafunzi wote 595,816 wa Kidato cha Nne ambao leo mnaanza mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari katika shule za sekondari 5,868 nchini. Mwenyezi Mungu Mtukufu awajalie utulivu mfanye na mkamilishe vyema hatua hii muhimu kwenye maisha yenu.
*Ninawaombea pia mwendelee kuwa na nidhamu, upendo na bidii katika hatua zinazofuata. Serikali itaendelea kuhakikisha ndoto zenu zinapata nafasi ya kukua na kustawi kwa manufaa yetu sote."

Vijana wote wa Kitanzania tunaungana na Rais wetu Dkt. Samia kuwatakia heri wanafunzi wote wa Tanzania wanaoanza mitihani yao leo. Mafanikio yenu ni fahari ya taifa letu, Mungu awabariki sana 🇹🇿

#KazinaUtuTunasongaMbele