UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

KAWAIDA AHUDHURIA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CCM

30 Nov, 2025 86 Machapisho
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Mohammed Kawaida, ameungana na viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kikao hicho, ambacho kimefanyika kisiwani Unguja, ni sehemu muhimu ya mnyororo wa maamuzi ya juu ya chama, kikiwa na lengo la kuimarisha uongozi na mwelekeo wa kisiasa wa CCM na Taifa kiujumla kuelekea utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.

Katika ajenda zake kuu za leo, Kamati Kuu imepitisha uteuzi wa wagombea wa CCM kwa nafasi za Umeya wa majiji, manispaa, pamoja na wenyeviti wa halmashauri za miji na wilaya, hatua inayotafsiriwa kama mwendelezo wa usimamizi makini katika kuhakikisha wananchi wanapata viongozi bora.

Ushiriki wa Ndugu Kawaida katika kikao hiki unadhihirisha nafasi muhimu ya vijana ndani ya CCM na mchango wake katika kujenga  viongozi mahiri na wenye maono ya kuendeleza misingi ya chama na Taifa kiujumla

#KazinaUtuTunasongaMbele