RAIS SAMIA ATWAA TUZO YA KIMATAIFA YA MAJI
Johannesburg, Afrika Kusini – 14 Agosti 2025:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Maji – Presidential Water Changemakers Award 2025 na Global Water Partnership kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika. Hafla ya tuzo hiyo imefanyika katika Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Afrika (AU–AIP Africa Water Investment Summit 2025) unaoendelea jijini Johannesburg kuanzia tarehe 13–15 Agosti 2025.
Tuzo hii imetolewa kwa kutambua mchango wa kipekee wa Rais Dkt. Samia katika kuongoza mageuzi makubwa ya sekta ya maji nchini Tanzania, hatua ambazo zimeboresha upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi wa mijini na vijijini.
Chini ya uongozi wake:
- Upatikanaji wa maji vijijini umeongezeka kufikia 79.6%
- Upatikanaji wa maji mijini umefikia 90%
- Miradi mikubwa 1,633 ya usambazaji maji imekamilika
- Vituo vipya vya maji 107,819 vimejengwa
- Zaidi ya wananchi milioni 12 wamenufaika moja kwa moja
- Vijiji 196,160 vimefikiwa na huduma ya maji
Mageuzi haya yameiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kama mfano wa taifa linalowekeza kwa vitendo katika huduma za kijamii, hususan maji safi na salama.
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.