UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUM CHA KAMATI KUU YA CCM

30 Nov, 2025 42 Machapisho
Unguja, 29 Novemba 2025 — Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika kisiwani Unguja, Zanzibar.

Kikao hicho muhimu, kilichowakutanisha viongozi wakuu wa chama, kimejadili masuala ya kimkakati yanayohusu  utekelezaji wa shughuli za chama katika ngazi mbalimbali za uongozi kwa maendeleo ya Taifa letu la Tanzania. 

Miongoni mwa maamuzi makuu yaliyofikiwa, Kamati Kuu imepitisha uteuzi wa wagombea wa CCM kwa nafasi za Umeya wa majiji, manispaa, pamoja na wenyeviti wa halmashauri za miji na wilaya. Uamuzi huo unatajwa kuwa sehemu ya kuweka viongozi bora katika jamii .
Uongozi wa Rais Samia katika kikao hiki unaendelea kudhihirisha msimamo wake thabiti wa kujenga CCM imara, yenye misingi ya uwajibikaji, umoja na ustawi wa wananchi