UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

RAIS SAMIA AMEWEKA NGUVU KUBWA KATIKA KUIMARISHA ELIMU YA VETA NCHINI TANZANIA

30 Nov, 2025 62 Machapisho
Kagera — Ijumaa ya tarehe 28 Novemba 2025, Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Kagera (VETA Kagera) kiliandika historia mpya kwa kufanya Mahafali yake ya pili, tukio lililofanyika katika viwanja vya chuo hicho vilivyopo Kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini. Mahafali hayo yameendelea kuthibitisha kasi ya ukuaji wa elimu ya ufundi stadi nchini chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa wageni waliohudhuria alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Burhan, ambaye aliwawakilisha vijana wa CCM na kutoa hotuba yenye uzito wa maendeleo, uzalendo na hamasa ya kitaifa.

“VETA Kagera ni alama ya uwekezaji wa kizazi kipya uliofanywa na Rais Samia,” — Faris Burhan

Katika hotuba yake, Faris Burhan alisisitiza kuwa VETA Kagera ni moja ya vielelezo vinavyoonekana vya namna Serikali ya Awamu ya Sita imeweka nguvu kubwa katika kuboresha elimu ya ufundi nchini Tanzania.
Amesema ujenzi wa chuo hicho, maboresho ya miundombinu, uwepo wa vifaa vya kisasa na walimu walioandaliwa vizuri ni sehemu ya dhamira ya wazi ya serikali kumwezesha kijana wa Kitanzania kuwa na ujuzi, ajira na uwezo wa kujiajiri.

Mafanikio yanayoonekana Kagera
Faris aliitaja VETA Kagera kama chuo kinachokua, kinachopendwa na jamii, na ambacho kimeendelea kutoa wahitimu wenye weledi kwa soko la ajira.
Ameipongeza menejimenti ya chuo kwa kukilea na kukisimamia vyema ili kiendelee kuwa kipya na bora kadri miaka inavyosonga.

Shukurani kwa wazazi, na hongera kwa wahitimu wa 2025
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Faris aliwashukuru wazazi na walezi kwa kuhakikisha vijana wao wanafika hatua ya kuhitimu.
Amesema taifa linahitaji vijana wenye: Nidhamu, Busara, Uzalendo. Maadili mema
Akiwatia moyo wahitimu, Faris alisema:-
 â€œMiaka mitano iliyopita nilikuwa kama ninyi. Leo nimerudi kama kiongozi kuwapongeza. Ninaamini miaka ijayo mtaendelea kupanda ngazi za mafanikio na kuitumikia Tanzania kwa uadilifu.”

Wito wa kulinda amani, umoja na utulivu wa nchi
Akitumia hadhara hiyo yenye mamia ya vijana, wazazi na wadau wa elimu, Faris alikumbusha umuhimu wa kulinda tunu za taifa.
Amesema amani, umoja na utulivu ndiyo msingi wa maendeleo ya kijana mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Aliwasihi vijana wa Kagera na Tanzania kwa ujumla kuwa mbali na vishawishi vinavyoweza kuvuruga utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa:
“Amani ndiyo mtaji wetu mkubwa. Bila amani hakuna elimu, hakuna ajira, hakuna maendeleo. Vijana tunapaswa kuwa mabalozi wa kulinda amani, upendo na umoja wa ataufa letu.”

Serikali ya CCM, vijana na mustakabali wa uchumi mpya
Faris alimaliza kwa kueleza kuwa chini ya Rais Dkt. Samia, serikali inaendelea kutekeleza mikakati ya kuimarisha elimu ya ufundi—ikiwemo ujenzi wa vyuo vipya, maboresho ya vifaa, na kuongeza fursa za mafunzo ya vitendo.
Amesema VETA Kagera ni sehemu ya muendelezo wa dira kubwa ya kujenga uchumi unaotegemea ujuzi, ubunifu na vijana wenye uwezo wa kuzalisha.