UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

REUBENS E. SAGAYIKA AAPA RASMI KUWA DIWANI KATA YA KALANGALALA, UVCCM WAMTAKIA HERI

02 Dec, 2025 29 Machapisho
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) unatoa pongezi  kwa Reubens E. Sagayika, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa, kwa kula kiapo cha kuwa Diwani wa Kata ya Kalangalala, Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

UVCCM inamtakia heri katika majukumu yake mapya ya kuwatumikia wananchi wa Kalangalala na Watanzania kwa ujumla. Uteuzi na kuapishwa kwake ni uthibitisho wa kuaminika kwa vijana na uwezo wao wa kushika nafasi za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikali.

Imani yake ni imani ya vijana—kuwa vijana wanaweza, vijana wana mchango mkubwa, na vijana ni nguvu ya taifa.

UVCCM tunampongeza sana na tunamtakia utumishi uliotukuka.