UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MWENEZI KENANI APOKELEWA KWA KISHINDO DAR ES SALAAM

06 Dec, 2025 39 Machapisho
 
Dar es Salaam, 06 Disemba 2025 — Ukumbi wa Diamond Jubilee ulibubujikwa na shamrashamra leo baada ya maelfu ya wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika kikao kazi cha kwanza cha Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Laban Kihongosi (MCC) na viongozi wa chama wa mkoa huo.

Ndugu Kenani, ambaye ameanza majukumu yake vyema kwa kasi ya kipekee, alipokelewa kwa kishindo kikubwa kilichoashiria matumaini mapya, mshikamano wa chama na nguvu ya kisiasa ya CCM katika jiji hilo. Viongozi mbalimbali wa ngazi zote za chama kuanzia matawi, kata, hadi mkoa  wamehudhuria, wakiwemo makatibu, wabunge, madiwani, na makada wa chama wamejitokeza kuunga mkono ajenda za uenezi na mafunzo anazozipeleka katika mikoa mbalimbali.

Kikao hiki cha kwanza jijini Dar es Salaam kinachukuliwa kama mwanzo wa safari mpya ya kuimarisha chama, kuongeza uelewa wa wanachama kuhusu Ilani ya CCM na kuongeza kasi ya uenezi wa mafanikio ya serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wameeleza kuwa mwitikio mkubwa wa leo unaonesha kuimarika kwa hamasa za chama na imani ya wananchi kwa ajenda ya maendeleo na maridhiano ya taifa.

“Dar es Salaam imeonyesha nguvu na umoja. Safari ya kuimarisha uenezi imeanza kwa kishindo,” alisema mmoja wa viongozi waliohudhuria kikao hicho.

Kikao hicho kimefungua ukurasa mpya wa mahusiano kati ya ofisi ya Mwenezi Taifa na viongozi na wanachama wote kuanzia tawi, shina na hadi mkoa na Dar es Salaam imeweka historia kama mkoa wa kwanza kumpokea Katibu Mwenezi mpya kwa mwitikio mkubwa wa aina yake.