UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

ATAKAYECHEZEA AMANI YA TAIFA LETU AWE ADUI YETU SOTE

21 Dec, 2025 25 Machapisho
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ametoa wito kwa vijana wote wa Kitanzania, viongozi na wananchi kwa ujumla kulinda, kutetea na kudumisha amani ya Taifa letu.
Amesisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu muhimu na ya msingi kwa ustawi wa Taifa, akibainisha kuwa yeyote atakayethubutu kuichezea amani hiyo hana nafasi katika jamii na anapaswa kuonekana kuwa adui wa wote. Kwa mujibu wake, maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa mazingira ya amani na utulivu.
Ujumbe huo umetolewa tarehe 21 Desemba 2025, mkoani Morogoro, wakati Ndugu Kawaida akizungumza akiwa Mgeni Rasmi katika Semina ya Viongozi Wapya wa Mikoa wa Taasisi ya Mama Aseme. Katika hotuba yake, amesisitiza kuwa jukumu la kulinda na kuimarisha amani ya Taifa ni wajibu wa kila kizazi, hususan vijana na viongozi waliopo madarakani.
Ameongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuhubiri mshikamano, uzalendo na maadili mema, huku wakikataa na kupinga kwa nguvu zote kauli, vitendo au ajenda zozote zinazoweza kuhatarisha umoja na amani ya Taifa.
Kwa upande wake, Taasisi ya Mama Asemewe imeendelea kuwa sauti imara ya kuelimisha na kuunganisha jamii, sambamba na kueleza ukweli kuhusu kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika kulinda amani, kuimarisha demokrasia na kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
#KazinaUtuTunasongaMbele