UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

TRILIONI 2.4 ZA RAIS DKT. SAMIA ZAAMSHA MUITIKIO MKUBWA KWA VIJANA WASOMI DAR ES SALAAM

23 Dec, 2025 21 Machapisho
Dar es Salaam, 23 Desemba 2025
Maelfu ya vijana wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika Hafla ya Ukaribisho wa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, chini ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC).
Hafla hiyo ilijumuisha mapokezi ya heshima, matembezi ya hamasa, na shangwe kubwa kutoka kwa vijana, ikionyesha mshikamano na imani yao kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika hotuba yake, Ndg. Kawaida alieleza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita imetenga Shilingi Trilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026, ikiwemo ongezeko la Bajeti ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Shilingi Bilioni 464 hadi 787, hatua iliyopokelewa kwa shangwe kubwa na vijana wasomi.
Hafla hiyo imeonyesha wazi kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaweka elimu na vijana katikati ya maendeleo ya Taifa, ikithibitisha dhamira ya kazi kwa utu na uwekezaji thabiti katika kizazi kijacho.