ZANZIBAR YANG'ARA : CCM GALA DINNER 2025 ZACHANGWA BILIONI 5.93
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza kwa kishindo hafla ya “CCM Gala Dinner 2025†iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip – Zanzibar, mnamo Agosti 17, 2025 kuanzia saa 11 jioni.
Baada ya mafanikio makubwa ya Gala Dinner ya Bara, sasa mwenge wa mshikamano na mshereheko umeendelea Visiwani Zanzibar kwa kishindo kikubwa. Hafla hii maalumu ya harambee imewaleta pamoja viongozi, vijana, wanachama na wadau mbalimbali walioujaza ukumbi kwa mapenzi ya dhati kwa chama chao kipenzi.
Katika tukio hilo la kihistoria, CCM imefanikiwa kuchangisha jumla ya Shilingi Bilioni 5.93, ikidhihirisha imani kubwa na mshikamano wa watanzania kuelekea ushindi wa chama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Mapenzi makubwa kwa viongozi wetu
Wanachama na wananchi walionekana kwa hamsa kubwa, wakimpa heshima na mapenzi ya dhati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakionyesha mshikamano na imani kubwa kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kukipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa uongozi wake bora. Vijana walijitokeza kwa wingi, wakichangia kwa hamasa kubwa na kuonyesha kuwa ndilo jeshi kubwa la ushindi wa CCM.
Hamasa ya kuchangia inaendelea
Mchango wa Zanzibar umekuwa ni ishara ya nguvu ya chama. Wananchi wanaendelea kuchangia kwa kasi kubwa kila kona ya nchi kuhakikisha chama kinajipanga ipasavyo kuelekea uchaguzi mwezi oktoba 2025.
👉 Jinsi ya Kuchangia kupitia Simu
-
Piga:
*150*50*1# -
Ingiza Control Number:
C02025 -
Weka Kiasi cha Mchango
-
Ingiza PIN yako kuthibitisha
📌 Michango itaendelea kupokelewa hadi Agosti 27, 2025 – kila mchango wako ni nguvu ya ushindi wa CCM na dhamira ya maendeleo kwa kila Mtanzania,Tuendelee kuchangia kwa kasi
Habari Zinazohusiana
TRILIONI 2.4 ZA RAIS DKT. SAMIA ZAAMSHA MUITIKIO MKUBWA KWA VIJANA WASOMI DAR ES SALAAM
23 Dec, 2025
Dar es Salaam, 23 Desemba 2025 Maelfu ya vijana wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika Hafla ya Ukaribisho wa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, chini ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC).
ATAKAYECHEZEA AMANI YA TAIFA LETU AWE ADUI YETU SOTE
21 Dec, 2025
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ametoa wito kwa vijana wote wa Kitanzania, viongozi na wananchi kwa ujumla kulinda, kutetea na kudumisha amani ya Taifa letu. Amesisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu muhimu na ya msingi kwa ustawi wa Taifa, akibainisha kuwa yeyote atakayethubutu kuichezea amani hiyo hana nafasi katika jamii na anapaswa kuonekana kuwa adui wa wote.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Rais wa Tanzania
14 Dec, 2025
Dar es Salaam | 14 Disemba 2025 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Antonio Guterres, ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa kielelezo cha amani, mshikamano wa kijamii na utulivu wa kisiasa barani Afrika na duniani, licha ya changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.