Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ndg. Halid Mwinyi, ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyoanzishwa na kuhakikisha kanuni za UVCCM zinasimamiwa ipasavyo katika kipindi cha uongozi wake.
Akizungumza jana tarehe 25 Agosti 2025 mbele ya maelfu ya vijana katika uzinduzi wa Kijani Ilani Chatbot, hotuba yake ya kwanza tangu kuteuliwa rasmi tarehe 23 Agosti 2025, Ndg. Mwinyi alimpongeza Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC), kwa kuendelea kuwa sauti ya vijana.
"Ameendelea kuwa na imani na vijana ikiwa ni pamoja na kutulea, kutusemea na kututetea," alisema Ndg. Mwinyi.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kumshukuru na kumpongeza Katibu Mkuu mstaafu, Ndg. Jokate Urban Mwegelo, kwa mchango wake mkubwa katika chama na jumuiya, akisisitiza kuwa mipango yake imesaidia kuimarisha UVCCM na kuwaunganisha vijana.
"Nimtakie kila la kheri na Mwenyezi Mungu amtangulie katika majukumu mapya atakayopangiwa," aliongeza.
Uzinduzi wa Kijani Ilani Chatbot umeelezwa kuwa ni hatua kubwa katika kuimarisha mawasiliano ya kidijitali kati ya UVCCM na vijana nchini, sambamba na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa njia rahisi na ya kisasa.
📌 #oktonatunatiki✅
📌 #tunazimazotetunawashakijani
📌 #kazinaututunasongambele