Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida, leo tarehe 27 Agosti 2025, ametembelea na kukagua maendeleo ya maandalizi ya Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam. Viwanja hivyo vinajiandaa kwa ajili ya tukio kubwa la Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) litakalofanyika kesho tarehe 28 Agosti 2025.
Katika ziara hiyo, Ndg. Kawaida aliambatana na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Halid Mwinyi, ambapo walipokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Cde. Nasra Mohammed.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Ndg. Kawaida aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria litakaloanza saa 12 asubuhi. Aidha, alibainisha kuwa katika uzinduzi huo Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, watawasilisha sera na ahadi za chama mbele ya Watanzania wote.
Kwa mujibu wa Ndg. Kawaida, maandalizi yote yamekamilika na kila Mtanzania anakaribishwa kushiriki tukio hili muhimu katika mustakabali wa taifa.
✅ #OktobaTunatiki
✅ #KazinaUtuTunasongaMbele
✅ #TunazimazoTtunawashaKijani