UVCCM yazindua “Kijani Ilani ChatBot
Dar es Salaam – Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Kawaida, ameongoza hafla ya uzinduzi wa Kijani Ilani Chat Bot, programu mpya ya kidijitali inayolenga kuongeza hamasa za kisiasa miongoni mwa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kawaida alisema kuwa kuimarishwa kwa kampeni za kidijitali ni hatua muhimu ya kuhakikisha vijana wanajitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura.
“Teknolojia hii mpya itakuwa nyenzo muhimu kwa vijana kupata taarifa sahihi za Ilani ya Chama, kujua vipaumbele na sera zetu, na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi,” alisema Kawaida.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa UVCCM Taifa, Khalid Mwinyi, alisisitiza umuhimu wa chat bot hiyo katika kuongeza uelewa wa vijana kuhusu dira na sera za chama.
“Tunakaribia uchaguzi mkuu, hivyo kampeni za kidijitali ni nyenzo isiyoepukika. Kupitia Kijani Ilani Chat Bot, vijana watapata fursa ya kujifunza na kuelewa zaidi dira ya chama chetu kuelekea uchaguzi,” alisema Mwinyi.
Aidha, Kawaida aliwataka vijana kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza wake Emmanuel Nchimbi, akiwapongeza kwa hatua ya kuchukua fomu za kugombea nafasi hizo.
Katika hotuba yake, alitoa pongezi kwa Katibu Mkuu mpya wa UVCCM Taifa, akimweleza kuwa ameandika historia ya kuwa kiongozi mdogo zaidi kushika wadhifa huo na kumhimiza kuhakikisha vijana wanatumia kikamilifu programu mpya ya Ilani ya Chama.
Akihitimisha hotuba yake, Kawaida alisisitiza vijana kupuuza upotoshaji wa mitandaoni unaohusiana na maandamano na badala yake wajikite katika maandalizi ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba.
“Ni wajibu wa kila kijana kuhakikisha anajitokeza kupiga kura. Tuwape mkono Rais wetu na chama chetu kwa vitendo,” alisisitiza.
Mwisho, aliwashukuru vijana wote waliohudhuria hafla hiyo kwa mshikamano wao na mwamko wa kuunga mkono jitihada za chama kupitia nyanja za kidijitali. bofya hapa kutembelea https://kijanichatbot.or.tz/
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.