UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

BALOZI NCHIMBI AHUTUBIA WANANCHI ISAKA, SHINYANGA

04 Sep, 2025 32 Machapisho
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo amehutubia wananchi wa Isaka mkoani Shinyanga baada ya wananchi kumzuilia kwa shangwe kubwa akiwa njiani kuelekea Kagongwa kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.

Katika hotuba yake, Balozi Nchimbi aliwaomba wananchi wa Isaka kumpa ridhaa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wagombea wote wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, ili kazi kubwa ya maendeleo iliyoanza chini ya CCM iendelee kuimarisha maisha ya Waisaka na Watanzania kwa ujumla.

Wananchi wa Isaka kwa umoja wao wamesema wazi:
“Oktoba ni Samia – Mitano Tena kwa Maendeleo!”