UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Balozi Dkt. Nchimbi Ahamasisha Wakazi wa Isaka Kuhakikisha Ushindi wa CCM Oktoba 29

04 Sep, 2025 86 Machapisho
Shinyanga, Septemba 3, 2025 – Mgombea Mwenza wa Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Alhamisi amewahutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Isaka, wilayani Kahama, Jimbo la Msalala, katika mkutano wa hadhara uliopambwa na hamasa kubwa za kisiasa.

Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi aliwanadi wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Ubunge hadi Udiwani, akimtaja kwa upekee Mabula Johnson Magangila, mgombea ubunge wa Jimbo la Msalala, pamoja na madiwani wa kata mbalimbali.

Akizungumza kwa msisitizo, Balozi Dkt. Nchimbi alisema kuwa anaendelea na ziara yake mkoani Shinyanga kwa lengo la kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030, ambayo imejikita katika kuboresha maisha ya wananchi, kuongeza fursa za ajira, kukuza huduma za kijamii na kuhakikisha maendeleo endelevu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Aidha, aliwaomba wananchi wa Shinyanga na Watanzania kwa ujumla kumpa kura za kishindo Mgombea Urais wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wabunge na madiwani wa chama hicho, ili kuhakikisha mwendelezo wa amani, utulivu, na maendeleo ya taifa.

“Mama Samia ni kiongozi mwenye dira ya maendeleo na anayo dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania wote. Kura zenu kwa CCM Oktoba 29 zitakuwa kura za kuendeleza ustawi na heshima ya nchi yetu,” 
Mkutano huo umekuwa sehemu ya mwendelezo wa kampeni za CCM zinazofanyika nchi nzima kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025