UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MBALIZI HAINA JAMBO DOGO, YAFUNIKA MAPOKEZI YA DKT. SAMIA

04 Sep, 2025 14 Machapisho
Mbeya, Septemba 4, 2025 – Mapokezi ya kishindo yamemsubiri Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya maelfu ya wakazi wa Mbalizi kujitokeza kwa wingi kumpokea na kushiriki naye katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo.

Dkt. Samia ameanza ziara ya siku mbili mkoani Mbeya kwa lengo la kuinadi Ilani ya CCM 2025–2030, ilani ambayo imebeba majibu ya kero na changamoto za wananchi, ikiwemo kuboresha huduma za afya, elimu, miundombinu, kilimo na ajira kwa vijana.

Wananchi wa Mbalizi wameonesha hamasa ya hali ya juu, huku wakipaza sauti za ushindi na kuonesha imani kubwa kwa CCM na mgombea wao wa urais. Mkutano huo umekuwa ni  ushahidi kwamba wananchi wa Mbeya wako tayari kumpa kura kwa kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.

Kwa mapokezi hayo ya leo, Mbalizi imeandika ukurasa mpya wa historia, ikionesha kwa vitendo  kuwa “hawana jambo dogo mbele ya Dkt. Samia – ni ushindi wa kishindo pekee Oktoba 29.”

📌 #OktobatunatikiFyuchaBilaStresi 
📌 #KazinaUtutunasongaMbele
📌 #TunazimazoteTunawashaKijani