UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Dkt. Nchimbi: Utafiti Maeneo ya Madini Utaongezeka kwa 50%

05 Sep, 2025 39 Machapisho
Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amesisitiza kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, endapo itapewa ridhaa ya kuingia madarakani tena, itahakikisha inatenga maeneo ya kutosha kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini na kuongeza kiwango cha utafiti wa madini kutoka asilimia 16 hadi 50.

Kauli hiyo ilitolewa leo Ijumaa, Septemba 5, 2025, wakati Dkt. Nchimbi akiwa mkoani Geita, katika wilaya za Mbogwe na Nyang’hwale, huku akiendelea na mwendelezo wa mikutano ya kampeni za CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

 "Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025/2030 imedhamiria kuongeza tija kwenye sekta ya madini, kwa kutenga maeneo kwa Wachimbaji Wadogo. Vile vile, Serikali ya Dkt. Samia inakusudia kuongeza kiwango cha utafiti wa madini kutoka asilimia 16 hadi kufikia 50," 

Ongezeko la maeneo ya wachimbaji wadogo na kiwango cha utafiti wa madini litatoa fursa kubwa kwa vijana wa Tanzania, kwani watapata ajira za moja kwa moja kwenye sekta ya madini, ujuzi wa kisasa katika utafiti na usimamizi wa madini, na uwezekano wa kuanzisha biashara ndogo ndogo zinazohusiana na madini. Hii itasaidia vijana kuwa na kipato thabiti, kujitegemea, na kuchangia maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi anashirikiana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakipeperusha bendera ya CCM, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ni sehemu ya kuhakikisha sekta ya madini inaleta tija, ajira, na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania has Vijana