UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

DKT.ASANTENI SANA NJOMBE, NIMESHUHUDIA UPENDO NA MAPOKEZI MAKUBWA

05 Sep, 2025 26 Machapisho
Maelfu ya wananchi wa Njombe wamejitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa kampeni uliofanyika mkoani humo.

Akihutubia wananchi, Dkt. Samia aliwashukuru kwa mapokezi makubwa na upendo waliomuonesha, akisema ni ishara ya imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake.

Katika hotuba yake, aliwaeleza wananchi mambo mazuri ambayo Serikali ya awamu ya Sita imeyatekeleza mkoani Njombe kwa mwaka 2020 -2025  na mipango mizuri zaidi itakayotekelezwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa mwaka 2025-2030.

Aidha, aliwaomba wananchi waendelee kuamini na kuiunga mkono CCM, huku akisisitiza kuwa Oktoba 29 ni siku ya kufanya maamuzi ya kishindo kwa kutiki chama Cha Mapinduzi kuanzia Urais, Ubunge na Udiwani .

#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi 
#KazinaUtuTunasongaMbele 
#TunazimaZoteTunawashaKijani