UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

IJUE ILANI YA CCM NGUZO ZA MAENDELEO YA TAIFA

10 Sep, 2025 40 Machapisho
Katika sekta ya nishati na miundombinu, Ilani ya CCM inalenga kupeleka umeme vijijini, kujenga barabara, madaraja, reli na bandari, Hatua hizi ni injini ya ukuaji wa uchumi na zinaunganisha wananchi wote bila kubagua.

Kwa upande wa afya, kipaumbele kimewekwa katika kuimarisha huduma za msingi, kujenga vituo vya afya, hospitali za kisasa na nyumba za watumishi, Lengo ni kuhakikisha kila Mtanzania, popote alipo, anapata huduma bora na za haraka ili kulinda afya ya jamii na kuongeza nguvu kazi ya taifa.

Katika usafirishaji, Ilani imejipanga kuongeza uwekezaji kwenye barabara kuu, stendi za kisasa, reli ya kisasa (SGR) pamoja na mabasi yaendayo haraka, Hatua hizi zitapunguza gharama za safari, kuongeza ufanisi wa biashara, kurahisisha safari za wananchi na kufungua fursa za kibiashara mikoa yote nchini.

#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatikiFyuchaBilaStresi
#NchiImetuliaHatunaDeniNaSamia