UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, ili kuendelea na kampeni za CCM za kunadi sera za CCM

19 Sep, 2025 11 Machapisho
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi•

(CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, ili kuendelea na kampeni za CCM za kunadi sera za chama hicho.
Dkt. Nchimbi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songea leo Septemba 19, 2025, na kupokelewa na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Ruvuma.

Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni za mgombea mwenza mkoani Ruvuma, Dkt. Nchimbi atafanya mikutabo ya kampeni katika maeneo ya Litui, Mbamba. Bay (Nyasa), Songea Mjini na Madaba.