UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MBINGA, SERIKALI YA CCM YAAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI

21 Sep, 2025 19 Machapisho
🗓️ 21 Septemba 2025
📍 Mbinga-Ruvuma

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itaendelea kuwatumikia wananchi wa Mbinga kwa kuhakikisha inasogeza karibu huduma muhimu za kijamii na kiuchumi, ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara vijijini na mijini, kuimarisha sekta ya afya kwa kujenga na kuboresha vituo vya kutolea huduma, pamoja na kuongeza fursa za elimu kwa watoto wa familia zote. Alisema Dkt Samia Suluhu Hassan 

Vile vile Viongozi wamesisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kusikiliza kero zao kwa uwazi, na kuhakikisha kuwa rasilimali za taifa zinawanufaisha wote kwa usawa ili kukuza ustawi na kupunguza changamoto za kiuchumi zinazowakabili wakazi wa wilaya ya Mbinga na mkoa kwa ujumla.

#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#KaziNaUtuTunasongaMbele