UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SOMBI ASHIRIKI KAMPENI NZEGA MJINI,

22 Sep, 2025 56 Machapisho
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC),ameshiriki  Kampeni na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, na wagombea  Ubunge Jimbo la Bukene, Nzega Vijijini na Nzega Mjini  pamoja na kuwaonbea kura wagombea Udiwani wa CCM.

Ndugu Rehema Sombi amewaombea kura wagombea hao wa CCM katika Uzinduzi wa Kampeni uliofanyika Nzega Mjini  Mkoa wa Tabora  Leo Septemba 21, 2025.

Katika Uzinduzi huo wamehudhuria maelfu ya Wananchi kutoka sehemu mbalimbali , viongozi na wanachama wa CCM huku Mratibu wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi CCM) kanda ya Kati na Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Dkt. Bashiru Ali, akiwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Nzega Mjini .

Kwa upande mwingine Komredi Sombi amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili wagombea hao wapate kura nyingi za kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025. Amesisitiza  Umoja na Mshikamano miongoni mwa wananchi huku akisema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndio Chama pekee ambacho kinashughulika na kutatua changamato za wananchi kwani kupitia  ilani ya 2025 - 2030 imeainisha vipaumbele ambavyo kupitia wagombea hao wananchi watapata miradi Mingi ya Maendeleo Kwani ni ilani bora na inapimika.

#oktobatunatiki✅✅ 
#KazinaUtuTunasongaMbele 
#fyuchabilaStresi
#TunazimaZoteTunawashaKijani