UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SOMBI ATETA NA VIJANA WA KAHAMA AWATAKA KUWA MSTARI WA MBELE KUZISAKA KURA ZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.

22 Sep, 2025 24 Machapisho
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndugu Rehema  Sombi amekutana na Vijana UVCCM   Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga Jana  Septemba 20, 2025 katika Ofisi za CCM Wilaya huku akiteta nao kuhusu wajibu wao wa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu Pamoja na kuhamasisha wengine wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

Aidha amewaomba Vijana kuwa mstari wa mbele kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili  kuhakikisha wagombea wote wa CCM ikiwemo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, wagombea Ubunge pamoja madiwani wanaibuka kidedea kwa  kura nyingi za kishindo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025. Pia ameelezea jinsi Ilani ya 2025-2030 ilivyobeba agenda ya Maendeleo kwa wananchi hivyo Vijana ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kupiga kura ili Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiendelee kushika Dola na kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.

#tunazimazotetunawashakijani
#OktobatunatikiFyuchaBilaStresi
#TunazimaZoteTunawashaKijani