SAMIA SCHOLARSHIP NI UFADHILI WA BURE KABISA SIO MKOPO
24 Sep, 2025
25 Machapisho
Kibaha, pwani.
23/09/2025
Mkuu wa idara ya uhusiano wa Kimataifa vyuo na vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg Emanuel Martine* leo tarehe 23.09.2025 akiambatana na Mwenyekiti wa UVCCM vyuo na vyuo Vikuu mkoa wa pwani Ndg Mwanaidi Khamis Ramadhani amefanya mazungumzo na waalimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari kibaha ambapo alipita kuwapa salamu za upendo za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Samia Suluhu Hassan.
Ndg Martine ametumia fursa hiyo kuwaambia wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita kuwa Dkt Samia Suluhu Hassan anawapenda wanafunzi na wazazi na walezi wa wanafunzi kwani ameanzisha mifuko ya ufadhili wa bure katika masomo ya sayansi, mifuko hiyo ni
1. SAMIA SCHOLARSHIP- huu ni ufadhili wa asilimia mia kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi, huu sio mkopo wa chuo ni ufadhili wa bure kabisa.
2. SAMIA EXTENDED PROGRAM- huu ni ufadhili wa kusoma nje ya nchi katika vyuo vya umahiri Duniani katika mambo ya Data sayansi na akili unde
3. SAMIA INNOVATION FUNDS
Pia Dkt Samia ameongeza bajeti ya Bodi ya mikopo ili wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita waweze kupata mikopo ya chuo
Awali kabla ya kupita shule ya sekondari kibaha Ndg Emanuel Martine alipata wasaa wa kuzungumza na Viongozi wa UVCCM vyuo na vyuo Vikuu mkoa wa pwani wakiongozwa na Ndg Mwanaidi khamis Ramadhani pamoja na timu ya ushindi ya vyuo na vyuo vikuu mkoa wa pwani na kuwataka kuendelea kutafuta kura za CCM.
Ndg Emanuel Martine amewasisitiza wanavyuo kuzitafuta kura za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan mtu kwa mtu, simu kwa simu, mitaa kwa mitaa, nyumba kwa nyumba, vijiwe kwa Vijiwe na makundi kwa makundi ili kuhakikisha Kura za Dkt Samia Suluhu Hassan zinapatikana kwa wingi, Samia ashinde kwa kushindo (fact and figure)
Kwa upande wao, Wanavyuo wamekikubali Chama Cha Mapinduzi Kwa Kuwa kimewawekea Sera bora Kwa Wanavyuo Kupitia Ilani yake 2025/30 Iliyoelekeza Ongezeko la Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu pamoja na Uboreshwaji Mitaala ya Elimu utakaosaidia katika Kuongeza mianya ya Ajira na kujiajiri mara baada ya Kuhitimu CCM inawapenda wanavyuo wote wa vyuo vya kati na vyuo Vikuu
#OktobaTunatiki✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazaZoteTunawashaKijani
#WanavyuoChaguaCCMChaguaSAMIA
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.