UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SOMBI AZINDUA RASMI KAMPENI JIMBO LA DIMANI

24 Sep, 2025 30 Machapisho
Dimani – Zanzibar, 23 Septemba 2025:
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC), leo amezindua rasmi kampeni za CCM katika Jimbo la Dimani, Zanzibar.

Akizungumza na wananchi na wanachama waliojitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara, Ndugu Rehema alisema kuwa CCM ndicho chama pekee kinachoweza kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli na kuendelea kulinda maslahi ya Taifa.
MAFANIKIO YA ILANI YA 2020–2030 ZANZIBAR 
Katika hotuba yake, alieleza kuwa kupitia Ilani ya CCM 2020–2030, Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imefanikisha miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo:
  • Ujenzi wa shule mpya za kisasa.
  • Vituo vya afya vilivyo karibu na wananchi.
  • Masoko yenye hadhi ya kimataifa.
  • Barabara za lami zinazounganisha mjini na vijijini
Katika kampeni hizo, Ndugu Rehema aliwanadi wagombea wa CCM kwa Jimbo la Dimani:
  • Ndugu Nabil Ahmed Abdillah – Mgombea Ubunge.
  • Ndugu Mwanaasha Khamis Juma – Mgombea Uwakilishi.
  • Wagombea Udiwani wa kata mbili za Dimani."
WITO KWA WANANCHI
Aidha, aliwaombea wananchi wa Dimani kura kwa wagombea wote wa CCM, akisisitiza umuhimu wa kumchagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025.

Ndugu Rehema pia aliwataka wananchi kudumisha amani, mshikamano na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi.
#SautiYenu
#OktobaTunatiki
#fyuchabilastres
#KaziNaUtuTunasongaMbele