Rais Dkt. Mwinyi Apokea Pole Kufuatia Kifo cha Kaka Yake
26 Sep, 2025
12 Machapisho
Zanzibar, 26 Septemba 2025 – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea salamu za pole kufuatia kifo cha kaka yake mpendwa, Marehemu Abbas Ali Mwinyi, kilichotokea jana tarehe 25 Septemba 2025.
Katika kuonesha mshikamano wa kitaifa na upendo wa kidugu, viongozi mbalimbali wa ngazi za juu walifika nyumbani kwa familia ya marehemu huko Bweleo, Mkoa wa Mjini Magharibi, kutoa mkono wa pole na rambirambi.
Uongozi wa Kitaifa Wajumuika
Miongoni mwa viongozi walioungana na Rais Mwinyi ni:
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
- Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Mashaka Biteko
- Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu
- Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
- Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid
- Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro
- pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa Serikali, chama na taasisi za dini.
RATIBA YA MAZISHI
Kwa mujibu wa familia, Marehemu Abbas Ali Mwinyi atasaliwa katika Masjid Jamia Zinjibar, Mazizini mara baada ya Sala ya Ijumaa, kisha kuzikwa Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja, leo tarehe 26 Septemba 2025.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Habari Zinazohusiana
KURA YANGU SAUTI YANGU
26 Oct, 2025
Ni haki yangu kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025
KAWAIDA: "WATAKE WASITAKE CCM ITASHINDA KWA KISHINDO KIKUBWA TAREHE 29"
26 Oct, 2025
Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa komredi Mohammed Ali Kawaida akizungumza na wananchi walio jitokeza kwa wingi katika Ufungaji wa Kampeni Jimbo la Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MARTINE AHAMASISHA WAPIGA KURA KUBEBA KADI ZAO OKTOBA 29 NA KUTIKI KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
26 Oct, 2025
Dar es Salaam, Oktoba 25, 2025 Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa Vyuo na Vyuo Vikuu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Emanuel Martine, amewahamasisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wateja na wadau mbalimbali wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025, wakichagua kwa kishindo wagombea wote wa CCM.