UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

π—™π—œπ—₯𝗦𝗧 π—§π—œπ— π—˜ π—©π—’π—§π—˜π—₯𝗦 π—žπ—”π—§π—”π—©π—œ π—ͺ𝗔𝗣𝗒 𝗧𝗔𝗬𝗔π—₯π—œ π—žπ—¨π—§π—œπ—žπ—œ π—’π—žπ—§π—’π—•π—” π—žπ—ͺ𝗔 π——π—žπ—§. π—¦π—”π— π—œπ—”

28 Sep, 2025 32 Machapisho

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa na pia Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM kutoka Mkoa wa Katavi, Eng. Debora Joseph Tluway, amekutana na vijana wapiga kura wapya walioshiriki kongamano la mbio za Mwenge lililofanyika katika Halmashauri ya Mpimbwe, Mkoa wa Katavi.

Katika kongamano hilo, Eng. Debora aliwapatia vijana elimu kuhusu mchakato wa upigaji kura, huku akisisitiza umuhimu wa kuchagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama nguzo ya maendeleo ya Taifa. Alisisitiza kuwa kura ya vijana ndiyo nguzo ya kulinda amani, mshikamano, na maendeleo endelevu yaliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Washiriki wa kongamano hilo walionesha shukrani zao kwa Serikali ya Dkt. Samia kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sekta ya elimu wilayani humo. Walibainisha kuwa ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa pamoja na elimu bila malipo hadi kidato cha sita ni neema kubwa kwa watoto wa Kitanzania na kielelezo cha uongozi wenye kujali maisha ya wananchi.

Aidha, vijana hao wapiga kura wapya waliapa kwa sauti moja kuwa ifikapo 29 Oktoba 2025 watamtikia kura ya NDIO Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan sambamba na wagombea wote wa CCM katika ngazi zote, wakisisitiza kuwa maendeleo yanayoonekana sasa ni sababu ya kuipa CCM ushindi wa kishindo 

#OktobaTunatikiβœ…βœ…βœ…
#FyuchaBilaStresi
#KazinaUtuTunasongaMbele