UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

MWAKITINYA, MWANRI MGUU KWA MGUU MITAANI KUZISAKA KURA ZA DKT. SAMIA

28 Sep, 2025 62 Machapisho

Kahama, Shinyanga
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara, Ndg. Mussa Peter Mwakitinya , leo 28 Septemba 2025 ameungana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Tabora, Ndg. Aggrey Mwanri, katika harakati za kusaka kura za kishindo kwa ajili ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika matembezi na mikutano ya mitaani, viongozi hao waliungana na wananchi wa Kahama na kuwasisitizia umuhimu wa kuendelea kuipa CCM ridhaa ya kuongoza nchi, wakibainisha kuwa utekelezaji wa Ilani ya CCM umeleta matokeo chanya yanayoonekana kwa macho ya kila Mtanzania.

Wananchi wa Kahama kwa upande wao walionesha kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyoletwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Dkt. Samia. Wameahidi kwamba ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025, watamtikia kura ya NDIO kwa kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wote wa CCM kuanzia ngazi ya ubunge hadi udiwani.

#OktobaTunatikiāœ…
#TunazimaZoteTunawashaKijani
#KazinaUtuTunasongaMbele