UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

SAMIA EXTENDED PROGRAM: WANAFUNZI KUTAFUTIWA VYUO VYA UMAHIRI DUNIANI KWA UFADHILI WA DKT. SAMIA

29 Sep, 2025 27 Machapisho

Mbeya, 29 Septemba 2025
Katika mwendelezo wa ziara zake za kukutana na makundi mbalimbali ya vijana na wanavyuo, Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg. Emanuel Martine leo amekutana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza, Mkoa wa Mbeya.

Akiwa mbele ya wanafunzi hao, Ndg. Martine amewataka  kuongeza bidii katika masomo ili kujiweka kwenye nafasi ya kunufaika na mpango kabambe wa SAMIA EXTENDED PROGRAM. Kupitia mpango huu, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan itawatafutia wanafunzi wenye ufaulu bora nafasi za masomo katika vyuo vikuu vya umahiri duniani kwa ufadhili kamili wa serikali.

Aidha, Martine alisisitiza kuwa Dkt. Samia ni Kiongozi mwenye moyo wa kipekee, kiongozi anayegusa maisha ya kila kijana na kila Mtanzania. Ni kiongozi anayeweka elimu, ustawi na maendeleo ya vijana mbele kama injini kuu ya kulijenga Taifa bora lenye matumaini na maendeleo endelevu

#OktobaTunatiki✅✅
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TunazoZoteTunawashaKijani
#WanavyuoChaguaCCMChaguaSAMIA