UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

BULUGU ATOA ELIMU JINSI YA KUPIGA KURA.

09 Oct, 2025 15 Machapisho
🗓️ Tarehe 08 Oktoba 2025
📍Mufindi-Iringa

Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Bulugu Magege, ameendelea na ziara ya kuhamasisha wananchi wa Mufindi hususani vijana wa Jimbo la Mafinga Mjini, kujitokeza kwa wingi Tarehe 29 Oktoba 2025 kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wagombea wote wa CCM. 

Akiwa katika Mitaa, Masoko na Vijiweni Magege amesisitiza vijana kuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea kura za CCM, huku akitoa elimu ya namna sahihi ya kupiga kura kwa mifano, akibainisha umuhimu wa kuhakikisha tiki inamweka mgombea wa CCM pekee, Ameeleza kuwa serikali ya Dkt. Samia Imeleta Mageuzi Makubwa katika elimu, afya, barabara na umeme, jambo linaloleta matumaini mapya kwa Watanzania.

#OktobaTunatiki âś…
#KazinaUtuTunasongaMbele
#TokaNitokeTukatiki âś…