UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

🗓️BILA CCM MADHUBUTI NCHI YETU ITAYUMBA

10 Oct, 2025 24 Machapisho
📍 Tarehe 10/10/2025
⏰Butiama-Mara

Akiwa katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika leo Butiama Mkoani Mara, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza kwa msisitizo mkubwa kuwa uimara wa Taifa letu unategemea Uimara wa CCM. 

Amesema chama hiki kimekuwa nguzo kuu ya amani, umoja na maendeleo tangu kupatikana kwa uhuru, na bila misingi imara ya CCM, nchi inaweza kuyumba kisiasa na kiuchumi Dkt. Samia amewataka Watanzania wote kuendelea kukiamini na kukiunga Mkono CCM kwa vitendo, hasa kwa kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kumpigia kura ili kuendeleza safari ya maendeleo yenye Uthabiti, Utulivu na Matumaini Kwa Wote.

#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki