UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Dkt. Hussein Ali Mwinyi asema atayatekeleza Mambo Matatu Muhimu Kwa Vijana

10 Oct, 2025 14 Machapisho
Kusini Unguja, Zanzibar – Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameyataja mambo matatu ambayo atayatekeleza kwa vijana endapo atachaguliwa katika uongozi ujao.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na vijana wa vyuo vikuu na makundi mbalimbali katika Chuo cha Mafunzo ya Vijana Tunguu, kilichopo Wilaya ya Kusini Unguja, mkoa wa Kusini Unguja.

Dk. Mwinyi amesema kuwa vijana wanahitaji fursa katika maeneo matatu muhimu: elimu, ajira na nafasi za uongozi.

"Tulipoingia tulikuta bajeti ya elimu ni shilingi bilioni 80 tu, sasa tumeongeza hadi shilingi bilioni 864, hivyo kipaumbele cha kwanza ni elimu ili vijana wetu waelimike. Kwa upande wa ajira, tumeahidi kutoa nafasi za ajira 350,000, na safari hii tutaongeza idadi hiyo zaidi kwa ajili ya vijana. Na fursa ya tatu ambayo vijana wanahitaji ni nafasi za uongozi, ambapo tutatoa nafasi za vijana katika uongozi wa serikali," alisema Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Vijana waliohudhuria mkutano huo wameshuhudia kauli hizi kwa furaha kubwa, wakionyesha hamasa ya kushirikiana na Dk. Mwinyi kuhakikisha kwamba vijana wanapata fursa na ushiriki mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar.

#KazinaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki
#TokaNitokeTukatiki