UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Banda la UVCCM Linaendelea Viwanja vya Uhindini

14 Oct, 2025 11 Machapisho
UVCCM imeendelea kutoa elimu kwa vijana katika viwanja vya Uhindini Jijini Mbeya, katika maonesho ya Wiki ya Vijana kitaifa  yanayoendelea. UVCCM imeendelea kuelimisha vijana namna sahihi ya kupiga kura za Mgombea wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia mfano wa karatasi ya kura, pamoja na umuhimu wa kushiriki uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, na kuchagua wabunge na madiwani wa CCM.

Vijana pia wameendelea kupewa elimu ya amani na utulivu wa Taifa, umuhimu wa uzalendo na jinsi ya kutumia haki zao za kidemokrasia kwa njia salama kupiga kura. Huduma zingine ni pamoja na usajili wa kielektroniki wa wanachama wa CCM, urejeshaji wa namba za kielektroniki kwa waliopoteza, na elimu ya mfumo wa Kijani Ilani Chatbot (Ilani ya CCM kidijitali kwa vijana). Huduma hizi zimevutia vijana wengi kuja kujifunza na kushiriki katika banda la UVCCM.

KAULI MBIU: NGUVU KAZI YA VIJANA KWA MAENDELEO ENDELEVU 💪🇹🇿

#KazinaUtuTunasongaMbele ✅
#TokaNitokeTukatiki ✅
#OktobaTunatiki ✅
#TunazimazoteTunawashaKijani