SERIKALI YA CCM KUJENGA TAWI LA JKCI GEITA MJINI
🗓 13 Oktoba 2025
📠Geita Mjini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa kiti cha Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akiinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi akiwa katika jimbo la Geita Mjini amewaeleza wananchi kuwa Serikali imejipanga kujenga tawi la JKCI ndani ya jimbo hilo ili kuwasogezea wananchi huduma ya matibabu ya moyo.
Hatua hii ni ushahidi tosha wa dira ya maendeleo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya bila kikwazo cha umbali wala gharama kubwa, Ujenzi wa tawi la JKCI Geita Mjini utakuwa chachu ya mageuzi makubwa katika sekta ya afya ya mkoa huo, kwani utapunguza rufaa nyingi kwenda Dar es Salaam, kuongeza ajira kwa wataalamu wa afya na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia huduma za kibingwa. Wananchi wa Geita sasa wanapaswa kuona hili kama ishara ya upendo wa kweli wa Serikali ya CCM kwao Serikali inayosikiliza, inayotekeleza, na inayoweka uhai wa wananchi wake mbele ya yote.
#OktobaTunatiki ✅✅✅
#FyuchaBilaStresi
#TokaNitokeTukatiki ✅
Habari Zinazohusiana
TRILIONI 2.4 ZA RAIS DKT. SAMIA ZAAMSHA MUITIKIO MKUBWA KWA VIJANA WASOMI DAR ES SALAAM
23 Dec, 2025
Dar es Salaam, 23 Desemba 2025 Maelfu ya vijana wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi katika Hafla ya Ukaribisho wa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, chini ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC).
ATAKAYECHEZEA AMANI YA TAIFA LETU AWE ADUI YETU SOTE
21 Dec, 2025
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ametoa wito kwa vijana wote wa Kitanzania, viongozi na wananchi kwa ujumla kulinda, kutetea na kudumisha amani ya Taifa letu. Amesisitiza kuwa amani ya Tanzania ni tunu muhimu na ya msingi kwa ustawi wa Taifa, akibainisha kuwa yeyote atakayethubutu kuichezea amani hiyo hana nafasi katika jamii na anapaswa kuonekana kuwa adui wa wote.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Rais wa Tanzania
14 Dec, 2025
Dar es Salaam | 14 Disemba 2025 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Mheshimiwa Antonio Guterres, ameipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa kielelezo cha amani, mshikamano wa kijamii na utulivu wa kisiasa barani Afrika na duniani, licha ya changamoto zilizojitokeza wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.