KAWAIDA: WATANZANIA TUTUMIE KIJANI ILANI CHATBOT KUTOKOMEZA UPOTOSHAJI
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC), amewataka Watanzania kutumia programu bunifu ya Kijani Ilani Chatbot kama nyenzo ya kupata taarifa sahihi kuhusu Ilani ya CCM na utekelezaji wake, ili kuongeza uelewa na kukabiliana na upotoshaji unaoenezwa na watu wasiolitakia mema Taifa.
Soma Zaidi
MWINYI: MFUMO WA ILANI KIJANI CHATBOT UNA MAMBO MATATU
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Ndg. Halid Mwinyi, ameeleza kuwa mfumo mpya wa kisasa wa Ilani Kijani Chatbot utarahisisha kwa kiasi kikubwa utoaji wa elimu kwa vijana wa Kitanzania juu ya fursa na mipango ya maendeleo iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2025–2030).
Soma Zaidi
ZANZIBAR YANG'ARA : CCM GALA DINNER 2025 ZACHANGWA BILIONI 5.93
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameongoza kwa kishindo hafla ya “CCM Gala Dinner 2025” iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip – Zanzibar, mnamo Agosti 17, 2025 kuanzia saa 11 jioni.
Soma Zaidi
RAIS SAMIA ATWAA TUZO YA KIMATAIFA YA MAJI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya Maji – Presidential Water Changemakers Award 2025 na Global Water Partnership kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika. Hafla ya tuzo hiyo imefanyika katika Mkutano wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji Afrika (AU–AIP Africa Water Investment Summit 2025) unaoendelea jijini Johannesburg kuanzia tarehe 13–15 Agosti 2025.
Soma Zaidi
CCM YAANZA HARAMBEE YA UCHAGUZI: WANANCHI WAIPOKEA KWA MIKONO MIWILI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumezindua rasmi harambee ya kuchangia kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kufanikisha kukusanya Shilingi Bilioni 86.31 katika uzinduzi uliofanyika Agosti 12, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Uzinduzi huu umepokelewa kwa shangwe na wananchi, wafanyabiashara, wadau wa maendeleo na wanachama wa CCM, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama, Rais Samia Suluhu Hassan. Katika harambee hiyo, Rais Samia alichangia Sh. Milioni 100, huku Rais wa Zanzibar,
Soma Zaidi
MAELFU WAJITOKEZA KUMSINDIKIZA DKT.SAMIA KUCHUKUA FOMU
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, wamechukua rasmi fomu za kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Tukio hilo limefanyika , Agosti 9, 2025, katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) zilizopo Njedengwa, Dodoma.
Soma Zaidi