UVCCM
Tafadhali subiri...
UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Habari & Matukio

Habari za CCM, Habari za Vijana, Habari za Maendeleo n.k

RAIS SAMIA AMEWEKA NGUVU KUBWA KATIKA KUIMARISHA ELIMU YA VETA NCHINI TANZANIA
30 Nov, 2025
00:00

RAIS SAMIA AMEWEKA NGUVU KUBWA KATIKA KUIMARISHA ELIMU YA VETA NCHINI TANZANIA

Kagera — Ijumaa ya tarehe 28 Novemba 2025, Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma Kagera (VETA Kagera) kiliandika historia mpya kwa kufanya Mahafali yake ya pili, tukio lililofanyika katika viwanja vya chuo hicho vilivyopo Kata ya Nyakato, Bukoba Vijijini. Mahafali hayo yameendelea kuthibitisha kasi ya ukuaji wa elimu ya ufundi stadi nchini chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Soma Zaidi
MWENYEKITI WA UVCCM NA MJUMBE WA KAMATI KUU, NDG. MOHAMMED ALI KAWAIDA, AONGOZA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM
26 Nov, 2025
00:00

MWENYEKITI WA UVCCM NA MJUMBE WA KAMATI KUU, NDG. MOHAMMED ALI KAWAIDA, AONGOZA KIKAO CHA BARAZA KUU LA UVCCM

Dodoma, 26 Novemba 2025 — Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM (MCC), Ndugu Mohammed Ali Kawaida, ameongoza kikao cha Baraza Kuu la UVCCM kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Soma Zaidi
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIWA KUSAFIRI
21 Nov, 2025
00:00

WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI KUKAMATWA NA KUZUIWA KUSAFIRI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji kumkamata na kuzuia hati ya kusafiria ya mkandarasi anayejenga mradi wa Kituo cha Ukaguzi cha Pamoja (One Stop Inspection Station) kilichopo Muhalala, mkoani Singida. Dkt. Mwigulu amesema Serikali ilimwamini mkandarasi huyo na kumpa jukumu la kutekeleza mradi huo muhimu wa kimkakati, ambao umesimama kwa zaidi ya miaka nane tangu mwaka 2016. Mradi huo, unaotekelezwa na kampuni

Soma Zaidi
RAIS SAMIA AWATAKIA HERI WANAFUNZI WANAOHITIMU KIDATO CHA NNE
17 Nov, 2025
00:00

RAIS SAMIA AWATAKIA HERI WANAFUNZI WANAOHITIMU KIDATO CHA NNE

Rais Dkt. Samia amewatakia heri na baraka wanafunzi 595,816 wa Kidato cha Nne wanaoanza mtihani wa kuhitimu leo tarehe 17 Nov, 2025 katika shule 5,868 nchini. Amesisitiza kuwa, pamoja na juhudi za Serikali za kujenga miundombinu, shule 305 mpya zinafanya mtihani huu kwa mara ya kwanza mwaka huu 2025 hatua inayothibitisha dhamira ya Serikali ya kupanua fursa za elimu bora kwa watoto wote wa Tanzania.

Soma Zaidi
RAIS DKT. SAMIA: WATANZANIA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LIDUMU KATIKA AMANI
16 Nov, 2025
00:00

RAIS DKT. SAMIA: WATANZANIA TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LIDUMU KATIKA AMANI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.

Soma Zaidi
Tanzania kunufaika na dolla million 20 kwa utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mbadiliko ya Tabia ya nchi
15 Nov, 2025
00:00

Tanzania kunufaika na dolla million 20 kwa utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na mbadiliko ya Tabia ya nchi

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazotarajia kunufaika na fedha kiasi cha hadi dola milioni 20 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia Mfuko wa Kukabiliana na Hasara na Uharibifu.

Soma Zaidi